Bongo MovieEvents

Steven Sandhu aandaa tamasha la filamu, funga mwaka

steven_sandhu
Mwigizaji Nyota wa filamu kutoka Maisha Plus Steven Sandhu ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika tasnia ya filamu swahiliwood, amekuwa kivutio katika filamu nyingi kutokana na staili yake ya nywele ambavyo huziweka.
Msanii huyo ameandaa tamasha la filamu pamoja na muziki na kulipatia jina la December Likizo Festival linatarajia kufanyika tarehe 31. December. 2012 jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Belinda Ocean Resort.

Steven kwa kushirikiana na kampuni ya yake ya Triple S Inc ndio watayarishaji wakuu wa tamashala hilo na anawakaribisha wadau wote wa burudani waende katika tamasha hilo la kihistoria, kwani kuna vitu vingi vitafanyika zaidi ya filamu tano zitakazozinduliwa. Alisema “kutakuwepo na Music,Fashion, Exhibition Arts na pia tamasha hili litakuwa kama sehemu ya kuwakutanisha wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbaliā€.

Baadhi ya wafanyabiashara wanaotarajiwa kuhudhuria December Likizo Festival ni kutoka nchi za Zambia, Afrika ya kusini, Zimbabwe, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Msanii huyo anawaomba wasanii kufika katika tamasha hilo kwa ajili ya kukutana na watayarishaji na wadau wa filamu kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kubadilishana mawazo na utalaamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents