Habari

Stewart Hall arejeshwa tena kama kocha wa Azam FC

Miezi miwili baada ya timu ya Azam FC kumtimua kocha Stewart Hall aliyekuwa amehamia kuifundisha timu ya Sofapaka ya nchini Kenya, klabu hiyo imempigia magoti na kumrejesha tena.

Uamuzi huo umechukuliwa na Azam FC ili kuziba pengo la kocha Boris Bunjak aliyetimuliwa Jumatatu hii.

Mmiliki wa Sofapaka Elly Kalekwa amesema hawezi kumzuia Hall baada ya kupewa ofa na klabu yake ya zamani ya Azam.

“It is true Azam have offered Stewart Hall an irresistible offer better than the one he had earlier in the team. We had discussions with him and I was very impressed since he is a coach who respects contracts and I have given him my blessings to make the decision he thinks suits him and we will not stop on his way to move back to Azam,” amekaririwa Kalekwa na mtandao wa Supersport.

“Stewart Hall will make up his mind since it is difficult to throw away such a big offer. Azam realised that mischievous people might have led the team astray leading to the coach sacking so they want him back.”

Hall anatarajiwa kuingia Dar es Salaam alhamis wiki hii kuanza kibarua chake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents