Bongo Movie

Stive Nyerere kuanza filamu ya Respect Nyerere Butiama

Stive_Nyerere_face_2

Mtaalamu wa kuiga  sauti ya Viongozi mbalimbali nchini, Stive Nyerere hivi karibuni amefungua kampuni yake mpya ya Nyerere The Power, kwa lengo la kufanya filamu za kisiasa na kiuchumi zaidi. Mwigizaji huyo ambaye kwa sasa anatamba na filamu ya Mr Presedent, ambayo inazungumzia maisha ya raisi wa jamuhuri wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete.


Stive  ameipasha BONGO5, kwamba tayari safari yao imeshaiva ya kwenda sehemu aliyozaliwa mwalimu Juliaus Nyerere Butiama, kwaajili ya filamu yake mpya ya Respect Nyerere. Amesema katika filamu hiyo ambayo itazungumzia mambo mbalimbali ya kisiasa na hotuba, alizokuwa akitoa mwalimu anamini itakuwa inamvuto zaidi ya ile ya Mr President.

Pia amesema kuanzia safari na taarifa zote za filamu hiyo, atazitoa hapa BONGO5 kwahiyo subiri picha zaidi kwaajili ya matukio ya filamu hiyo.

By Mo One’s

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents