Watanzania wenyewe tunaiua Bongo Flava

Ukitaka kuongelea wasanii wa RnB wanaong’ara hapa bongo basi ni lazima pia utamzungumzia Steve RnB. Steve ambaye aling’ara mara tu baada ya wimbo wa tabasamu wa Mr Blue kuwa hewani, kupitia wimbo huo aliweza kuonyesha ujuzi wake wa kughani mpaka kila mtu aliyeskiliza wimbo ule alifurahi na aliamini kweli stive anaweza.

Akiongea na bongo5.com Steve alisema

anafurahi kuona muziki wa bongo unavyoenda kwani kuna watu wanajitahidi kuuinua na pia kuna watanzania wanaourudsha nyuma hivyo kuufanya muziki wetu kushindwa kuwa wa kimataifa zaidi na badala yake kubaki kuwa ni wa hapa hapa bongo na labda Africa mashariki kidogo.

 

Steve alikamilisha usemi huu kwa kusema kuwa muziki wa bongo haukui kwa sababu ubunifu wa wasanii ni mdogo sana na media pamoja na wadau wakubwa kulimit wasaniii “unajua kwanini muziki wetu unabaki kuwa ni wa hapa hapa bongo tu na labda Africa Mashariki!?” alianza kwa kuuliza kasha akaendelea….. “….. kwanza kabisa wasanii hatuna ubunifu wa kutosha na ndio maana tunabaki kutamba bongo tu na kama tutatoka basi nsio nje ya Africa Mashariki, hii nikutokana na msanii akisikika tu kidogo basi anabweteka na kuona kama amefika kumbe pale ndio anatakiwa ajipange kwa jaili ya kusonga mbele”.

Kwa upande mwingine aliongeza kwa kusema media na wadau wakubwa wa huu muziki hapa bongo ndio wanaoua mziki kwa kuwalimit wasanii “kingine ni hawa wadau wakubwa pamoja na media, wanalimit sana wasanii kwa kuwalazimisha kuimba kile ambacho sio uwezo wao, yaani msanii analizimishwa kuimba kile ambacho sicho yeye anachotaka kukiimba kutoka moyoni na ndio maana hatufiki mbali.”
Stive ambaye anatesa nakibao chake cha one love akiwa amefanya kolabo na Baby boy kwa sasa anasoma katika chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM kilichopo jijini Dar es Salaam akiwa anachukualia IT ikiwa ni mwaka wa pili. Alimalizia kwa kusema wasanii warudi shule kuongeza elmu kwani muziki bila elimu ni sawa na hakuna kitu!.

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW