Michezo

Stoke City yamng’ang’ania Peter Crouch

Mwenyekiti wa klabu ya Stoke City, Peter Coates anaimani straika wake, Peter Crouch atasaini mkataba mpya wa miaka sita utakao muwezesha kuendelea kusalia katika timu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.

Straika wa Stoke City, Peter Crouch

Crouch mwenyye umri wa miaka 36, amefunga jumla ya mabao 57 katika michezo 200 aliyocheza toka ajiunge na Stoke mwaka 2011 huku mkataba wake ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

“Peter anafahamu kuwa tunathamini mchango wake katika kablu yetu siondani ya uwanja pekee bali hata katika maisha yake ya kawaida,” alinukuliwa Coates akizungumza kupitia Stoke Sentinel.

“Tunaimani tutakaa pande mbili na kuzungumzia hilo, tuna mahusiano mazuri na yeye tungependa amalize soka lake na sisi.”

Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Liverpool imefunga mabao matatu katika michuano ya ligi saba alizocheza msimu huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents