Burudani

Studio mpya ya Profesa Jay yakamilika, kuanza kufanya kazi hivi karibuni

Baada ya kupata mafanikio na heshima kupitia muziki rapper mkongwe Profesa Jay ameamua kujiunga na familia ya wasanii wanaomiliki studio zao wenyewe, anatarajia kufungua studio yake ya kutengeneza muziki hivi karibuni.

profesa Jay

Joseph Haule aka Profesa Jay ameiambia Bongo5 kuwa kila kitu kimekamilika upande wa vifaa vya studio ikiwa ni pamoja na ‘setup’ iliyofanywa na producer Duke lakini bado haijaanza rasmi kuifanya kazi.

“Nadhani wiki hii kila kitu kitakuwa kwenye pipeline sema kuna taratibu za kisheria ndio bado nazishughulikia lakini soon itaanza”. Alisema Jay.

Professa Jay ameahidi kutaja jina la producer atakayemfanyia kazi pamoja na jina la studio pale taratibu zote zitakapokamilika na kuwa tayari kuifungua rasmi.

Jay anakua miongoni mwa wasanii wanaomiliki studio zao za kurekodi Muziki Tanzania ambao ni pamoja na Dully Sykes, Quick Rocker, Mb Dogg, Benjamin wa Mambo Jambo, Juma Nature, Kikosi cha mizinga na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents