Habari

Suala la ubinafsishaji silipendi – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa suala la ubinafsishaji halipendi huku akisema hawezi kuwalaumu waliofanya hayo na hawezi kuacha kusema.

Akiongea na wananchi wa Itigi mkoani Singida leo mchana Rais Magufuli ambapo amezindua barabara ya Manyoni – Itigi – Chaya yenye urefu wa KM 89.3.

“Suala la ubinafsishaji mimi silipendi, siwezi nikawalaumu waliofanya haya lakini siwezi nikaacha kusema. Ni lazima niyatapike haya, nikikaa nayo nitapata presha na wale walioyafanya wakumbuke madhambi yao”,amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemaliza ziara yake katika mikoa minne.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents