Habari

Suala la walimu kukosa udhamini katika mabenki lafika bungeni

Naibu Waziri-TAMISEMI, Joseph Kakunda amesema kuwa hakuna dhamana mtumishi kukopa katika mabenki au taasisi zaidi ya dhamana ya mshahara wake kinachotakiwa mtumishi asiwe anadaiwa mikopo mingine.

Kakunda ameyasema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge Grace Victor Tendega aliyehoji kuwa,

Walimu wameukuwa wakikosa udhamini katika mabenki mbalimbali kutoka kutokuwa na mali, na hivyo alivyovisema Naibu Wazii ni vitu visivyohamishika kama viwanja, magari na vitu vingine na tunatambua hali za walimu wetu zilivyo Je serikali haioni haja kuwa ni wakati muafaka mifuko ya hifadhi ya jamii iweze kufanya dhamana kwa walimu wetu wakati wakiwa kazini na sio baada ya kustaafu?

“Karibu mabenki yote na taasisi zote hakuna dhamana zaidi ya mshahara wa Mtumishi kinachotakiwa mtumishi asiwe anadaiwa mikopo mingine hilo ndio jambo la msingi na kama mtumishi hadaiwi mikopo mingine anao uwezo wa kukopa na ataamua mwenye akope kwa kurejesha miaka mitatu u akope kwa kurejesha miaka 10 au akope kwa kurejesha miaka 25 ni yeye mwenyewe katika makubaliano ya sehemu yake kwahiyo napenda kuwasisitiza watumishi wote nchi nzima na Wakurugenzi wa Halmashauri ambao wako chini yangu nataka niwaambie kwamba mikopo hiyo ya watumishi ipo waingie katika makubaliano maalum na hizo taasisi na mabenki ili watumishi waweze kukopeshwa na wajenge nyumba zao binafsi,” amesema Kakunda.

“Kwanza naomba nisisitize kwamba kwenye jibu langu la msingi ile takwimu niliitaja kwa Bunge lako tukufu haikumaanisha walimu hao hawana makazi kabisa nilisema walimu hao katika either nyumba za kupanga au nyumba zao binafsi na sehemu ya kwanza ya swali lake kwamba kwanini jeshi la polisi kujenga nyumba za polisi nchi nzima, hilo naomba Mh. Naibu Spika lina kazi zake maalum waliojenga ukuta wa Mirerani sio Jeshi la polisi,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents