Michezo

Suarez amuomba msamaha Giorgio Chellinii kufuatia tukio la kumng’ata

MshambuliAJI wa timu ya taifa ya Uruguay na Liverpool ya Uingereza, Luiz Suarez sasa amemuomba msamaha mlinzi wa Italia Giorgio Chellinii kufuatia tukio la kumng’ata wakati timu hizo zilipokuwa zicheza mechi ya mwisho ya makundi huko Brazil.

Suarez-main

Suarez aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ‘Baada ya kuketi nyumbani na familia yangu na kutulia imenijia kuwa tukio la kumng’ata Chellini ni la kusikitisha na kwamba sitarudia tena. Ninajutia sana tukio hilo na ninamuomba msamaha Chellini, ukweli ni kwamba anauguza jereha la kuumwa baada ya kugongana naye katika mechi hiyo”

BrZNtsXCEAAXZGY

Suarez alimng’ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Uruguay ilipowalaza mabingwa hao wa zamani wa dunia 1-0 jumanne iliyopita. FIFA imeamuru asishiriki mechi yeyote ile kwa kipindi cha miezi minne mbali na kulipa faini ya pauni 65000. (£65,680).Awali katibu mkuu wa Fifa Jerome Valcke alimtaka Suarez atafute matibabu ya kisaikolojia wakati akitumikia marufuku hiyo.

Hii si mara ya kwanza wala hata ya pili kwa Suarez kukabiliwa na kashfa kama hii ya kuwauma wapinzani wake , msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic Aprili 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents