Sudan Kusini yamtangaza Abdelmalek kuwa kocha wa timu ya Taifa

Shirikisho la soka nchini Sudan Kusini limemteuwa, Aït Ahcene Abdelmalek kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.

Abdelmalek raia wa Algeria amepewa kibarua hicho cha kuinoa timu hiyo ya taifa ya Sudani Kusini (the Bright Stars) kwaajili ya maandalizi ya michuano mwaka 2019.

Mtihani wake wa kwanza atakao kabiliana nao ni kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika yatakaoyofanyika nchini Cameroon mwaka 2019 ambapo atakabiliana na timu ya taifa ya Mali mwezi Septemba mwaka 2018.

Wakati Sudani Kusini ilipoteza mchezo wake wa ufunguzi wa group C kwa jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Burundi mwezi Juni.

Abdelmalek si mgeni soka la Afrika kwani alishawahi kuifundisha timu ya taifa ya Burundi na Algeria lakini pia na Djoliba.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW