Habari

Sudan yamuomba Rais Magufuli kutatua mgogoro wao

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini, Rebecca Nyandeng Garang de Mabior.

_92889037_unnamed-1

Baada ya mazungumzo hayo, Bi. Mabior amesema yeye pamoja na ujumbe wake wamelazimika kufika Tanzania kuonana na Rais Dkt Magufuli kwa lengo la kumfahamisha hali halisi ya nchi ya Sudan ya Kusini.

“Tumefarijika kuwa hapa katika ikulu ya Tanzania na tuko hapa kumsihi Rais Dkt Magufuli kama Mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki, akishirikiana na viongozi wenzake wa jumuiya hiyo kuona namna gani wanaweza kutusaidia ili taifa la Sudan ya Kusini liwe taifa lenye amani. Hivyo hapa tunawakilisha vilio vya watu wa nchi yetu na kikubwa tunachokitaka ni amani katika nchi yetu na hiki ndicho kilio chetu, ” alisema.

Naye Rais Magufuli kwa upande wake amewasihi viongozi na wananchi wa Sudan ya Kusini kutafuta njia muafaka ya kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani na ili kuepuka machafuko yanayosababisha mateso kwa wananchi wa taifa hilo.

“Mama Rebecca hata mimi binafsi naumizwa na kile kinachoendelea katika nchi ya Sudani ya Kusini hivyo ningezisihi pande zote zinazotofautiana kumaliza tofauti zao kwa amani kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa la Sudani ya Kusini,” alisema.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents