Sugu akamatwa na kujidhamini

Inasemekana kwamba msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva Joseph Mbilinyi aka Sugu aka Mr II alikamatwa jana asubuhi katika ofisi za BASATA alipokuwa na Press Conference juu ya masuala ya muziki, na kwa sasa yupo mitaani akiwa ameachiwa huru kwa dhamana. [soma zaidi kusikiliza wimbo wa ANTIVIRUS]

Inasemekana kuwa alikamatwa na polisi baada ya mmoja wa viongozi wa redio flani ya hapa jijini kumshitaki kuwa yeye (MR II) anamtishia maisha na pia kwenye wimbo wake wa ANTIVIRUS. Na kwamba baada ya kukamatwa alipelekwa katika kituo cha polisi cha upelelezi kwa ajili ya mahojiano, lakini baada ya muda Mr II aliachiwa huru kwa kujidhamini yeye mwenyewe.

Aidha Msanii huyo ametakiwa kuripoti tena kesho katika ofisi hizo kwa mahojiano zaidi. Tutawaletea habari zaidi kesho.

Sikiliza wimbo wa Antivirus hapa chini

{youtube}hiMGe2HYq2o{/youtube}

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW