Burudani

Sugu amshtaki mama wa mtoto wake Faiza, anahisi anamharibu mwanae

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu amemshtaki aliyewahi kuwa mchumba wake Faiza Ally na aliyezaa naye mtoto kwa madai kuwa mwanamke huyo hana maadili na anahofia atamharibu mtoto wao. Sugu anataka kumchukua mtoto huyo na aishi naye (child custody).

ffffff

Faiza ameiambia Bongo5 kuwa baada ya siku chache zilizopita kupandishwa kizimbani na kujibu shtaka hilo, alisema yeye hawezi kukubali kumuachia Sugu mtoto huyo kwa kuwa yupo chini ya umri.

“Kweli Sugu amenipeleka mahakamani kumtaka mtoto,” amesema Faiza. “Mimi naona ni mtu anayekwepa majukumu kwa sababu chanzo cha yote nilikuwa namkata atulipie kodi ya nyumba, kwa sababu toka tuachane hajawahi kulipa kodi ya nyumba na siyo baba ambae anajali majukumu ya nyumbani kama inavyotakiwa.”

faiza-ally

“Kwahiyo nilivyoanza kumshauri kuhusu hilo akaniambia yeye anaweza kumchukua mtoto wake na mali zake anaweza kumlea mtoto wake. Sasa nilivyobishana naye kuhusu hilo wiki moja baadaye ndo likaja ili suala la KTMA ndio akalichukulia kama sababu ya kuweza kupeleka suala mahakamani kwa kudai sina maadili, kwahiyo nitammharibu mtoto. Kwahiyo kesho Jumanne ndio hakimu anatoa hukumu juu ya hili.

Lakini mtoto bado ni mdogo ana miaka miwili na kama miezi tisa bado mdogo anahitaji malezi yangu, pia hili suala nitalipeka ustawi wa jamii ili waangalie haki ya malezi ya mama kwa mtoto.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents