Aisee DSTV!

Sugu apigwa miezi mitano jela (+Video)

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, imewatia hatiani mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga na kuwahukumu kifungo cha miezi mitano jela.

Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26,2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite.

Sugu anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli. Ambayo wanadaiwa kuitoa Disemba 30 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge mkoani Mbeya.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW