Habari

Sugu awaomba viongozi kuutumia Mwezi Mtukufu kujitathmini

Mbunge wa Mbeya, Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa tiketi ya CHADEMA amewaomba viongozi nchini kuutumia mwezi mtukufu kujitathmini.

Akizungumza leo Mei 21, kwa mara ya kwanza Bungeni tangu atoke gerezani kwa msamaha wa Rais wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia Waislam wote mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhan.

“Naomba niwatakie ndugu zangu Waislam mfungo mwema, Kwa wale viongozi naomba muutumie Mwezi Mtukufu kujitathmini, sheria hii pamoja sheria mbovu za habari zinazowabana wananchi kupata habari pia zinatumika kufunga watu jela kisiasa kwa mfano mimi nilifungwa kwa kujadiliana na wananchi wangu kuhusiana na watu kupigwa risasi, watu kutekwa, maiti kuokotwa kwenye viroba watu kutokuwa na uhru wa kuongea n.k,Ni lini sheria hizi zitafutwa ili kulinda Katiba ya nchi hususani ibara ya 18? alihoji Sugu.

Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ aliachiwa huru gereza la Ruanda, Mbeya Mei 10 alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents