Burudani

Sugu kuizindua Anti Virus

PICT0034

Mwanamuziki na Mbunge wa Mbeya mjini mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, anatarajia kuzindua albamu ya Anti Virus, jumapili ijayo katika Usiku wa Sunday Night pale Bilicanas.  Akiongea na Bongo5, mratibu wake Fredy Maliki ‘Mkoloni’ alisema ilibidi waizindue siku ya Jumapili ya tarehe 20, lakini walisitisha kutokana na matatizo yaliyolikumba taifa kutokana na milipuko ya mabomu huko Gongo la Mboto.

Alisema kuzindua kwa albamu hiyo ya Anti Virus Vol 1 ni kujipanga kwa kuiandaa Anti Virus Vol 2, ambayo itashirikisha wasanii wale wale.

Anti Virus ni albamu ambayo ilishasambaa kwa watu wengi, kupitia Internet huku ikipatikana bure. Wasanii watakao kuwemo humo, ni Mapacha, Mkoloni, Sugu, na wengine wengi huku mgeni wao akiwa msanii mwenzao Saruti.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents