Michezo

Suleimani Matola amenifanya kuwa bora – Denis Richard

Golikipa wa klabu ya Simba SC, Denis Richard amezungumzia namna anavyojiamini na uwezo mkubwa aliokuwanao katika mchezo wa soka.

Golikipa wa klabu ya Simba SC, Denis Richard

Richard ambaye ni shabiki mkubwa wa golikipa wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Porto, Iker Casillas ameyasema hayo kupitia mtandao wa kijamii wa timu hiyo.

“Uwezo wangu nauwamini na hauwezi kuwa bora pasipo kupitia mafunzo na kuwa na mtu mwenye uwezo wa kuendeleza uwezo niliokuwa nao.

“Kwahiyo kipaji changu na uwezo wangu ni mwalimu ndiye atakaye endeleza, kuna makocha wawili sitokuja kuwasahau kwenye maisha yangu ya mpira kwa sababu wao ndio walionifanya mpaka nikawa na uwezo huu niliyokuwa nao”.

“Wakwanza sitomsahau Meja bakari yeye ndiye aliyenifanya nikatambua kipaji changu, na wapili ni Suleiman Matola alichangia mimi kuwa bora zaidi na kujulikana,” amesema mlinda lango huyo wa Simba.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents