Suma G akutana na MB Dogg feki

Msanii Suma G ambaye taarifa za kinoko zinamuelezea kama mkataji monde(Beer) maarufu miongoni mwa wasanii,amewashauri wasanii maarufu ambao hawajatoa video hata moja kwa sasa wafanye hivyo haraka ili kuepukana na matapeli wanaowaibia kazi zao.


Suma aliyasema hayo ktk mahojiano ya karibuni…kufuatia tukio la utapeli wa hali ya kutisha alilokutana nalo alipokuwa ziarani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Akiulezea mkasa huo..mtaalam huyo wa kukamata Monde alisema, akiwa mkoani Mwanza alisikia katika matangazo kuwa atafanya onyesho la pamoja na MB Dogg lakini walipoingia ukumbini alishangaa kumuona mtu anayeimba kibao cha ?Latifa? kuwa si MB Dogg anayemfahamu na wala hakuwa na muonekana wa kufanana na Mb hata kidogooo.

Akiendelea alisema…….Lakini kwa kuwa nilikuwa mbali na jukwaa na alikuwa akiimba kwa kufuatisha mashairi nyuma ya CD (playback), ilikuwa ngumu kumshtukia… lakini nikahisi kitu tofauti na nilipoenda pale na kumsogelea kwa karibu nikagundua Mb Dog ninayemfahamu.Nilipombana sawa sawa anieleze ni kwanini alikuwa akiwatapeli wananchi kwa kujitia Mb Dog?…alianza kutetemeka na kuniomba nimsitiri asije kuuawa na mashabiki wenye hasira.

Kwa kweli sikuwa na huruma naye, lakini wakati nikiwa katika harakati za kutaka kumchukulia hatua msanii huyo feki alinipotea katika mazingira ya kutatanisha na sikumuona tena.??

Suma akaongeza: ’Kama Dogg angekuwa na video, angeweza kudhibiti aina hii ya wizi.wa kishenzi’.Hahaha haya mnasikia wasanii namna matapeli wa mikoani kama sio vijijini wanavyojizolea mkwanja kutokana na watu tu kutowajua sura zenu? Duh hii kiboko mi sina la kusema hahahah

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW