Soka saa 24!

Suma Mnazareti awaza soko la nje

suma

MWANAMUZIKI  Sumail Salum ‘Suma Mnazareti’ kutoka pande za Manzese, Mabibo Makutano  amesema kwa sasa anaangalia soko la nje zaidi kuliko la ndani kwakuwa lengo lake ni kubuludisha na kupata mshiko, ilikuweza kukidhi mahitaji yake ya msingi.

 

 

Suma anasema kwa sasa ameshatoa nyimbo tatu ambazo ni Tofauti na Jana, Hisia za mtaa na Nyota ya mchezo, na nyingine nyingi zinakuja. amesema anafikiria zaidi nyimbo zake kupigwa Mtv Base na Channel O kuliko vyombo vya ndani kwakuwa mameneja wake ndivyo walivyotaka.

 

suma_mnazareti

Anasema zaidi ya kipaji cha kuimba pia anafanya kazi ya kushoot, video zake mwenyewe na kuzifanyia Editing, ha hii alifanya hadi kwa kazi za wasanii wengine kama wimbo Nahitaji wa P way aliomshirikisha Q jay (Ambaye sasa ni mlokole)

SUMA2

Anasema haogopi wingi wa wasanii kwakuwa kila msanii anakuja na uwezo wake na pia wanakuja na vipaji kuliko wakongwe, hivyo hiyo kwake ni kama changa moto, anasema pia wapo wengine wengi wanajua lakini wamekosa nafasi.

Alimalizia kwa kusema Vyombo za habari siku hizi vimekaa kibiashara kwakuwa ni vya watu binafsi, kwa hiyo malalamiko ya watu kwamba wanakuwa na upendeleo na mwanamuziki fulani ametoa fedha au hakutoa yeye haimuumizi kichwa. anasema huwezi jua chombo hivyo kimejipangaje katika mikakati yao, kwani huenda labda ulipe ndiyo upigiqwe nyimbo zako, kwakuwa ni chombo huria.

Hivi sasa anatarajia kuitambulisha staili mpya ya muziki ambao haujawahi kuibwa Afrika mashariki na kuachana kabisa staili ya Hip Hop za Kibongo bongo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW