Sumalee afiwa na baba yake mzazi, ashindwa kuhudhuria mazishi

sumalee

Hitmaker wa Hakunaga, Sumalee, amefiwa na baba yake mzazi, Mzee Sadick Iddi. Taarifa hizo zimetolewa na yeye mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Hata hivyo Sumalee ambaye yupo nchini Uingereza hatoweza kuhudhuria mazishi ya baba yake yanayofanyika leo mchana. Sababu ni kutokana tiketi yake ya ndege na visa kuchelewa toka katika ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Mwaka jana msanii huyo alifiwa pia na mama yake mzazi.Tunampa pole kwa msiba huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents