Sumaye ashindwa uchaguzi ndani ya Chadema, licha ya kuwa mgombea pekee wa unyekiti Pwani

Aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye ameshindwa kutetea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura ya hapana.

Image result for frederick sumaye chadema
Katika uchaguzi huo uliofanyika jana Alhamisi Novemba 28, 2019 mjini Kibaha Mkoa wa Pwani, Sumaye aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mwaka 1995 hadi 2005 amepigiwa kura 28 za ndio na 48 za hapana na kura moja imeharibika.

Inadaiwa kitendo cha kuchukua fomu za kuwania nafasi ya mwenyekiti wa Chadema ndiyo chanzo cha kushindwa kwenye uchaguzi mwenyekiti Kanda ya Pwani.

Chanzo Mwananchi

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW