Habari

SUMBAWANGA: Mvua kali yaua mtu mmoja na kuacha Kaya 336 bila makazi

Kaya zipatazo 336 katika kata ya Kipeta wilayani Sumbawanga hazina sehemu za kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa mapaa na kubomolewa na mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha usiku wa kuamkia jana mkoani Rukwa.

Mbali na nyumba za wananchi, maafa hayo pia yametokea katika Shule ya Sekondari ya Kipeta ambapo madarasa ya shule hiyo na nyumba tano za walimu zimeezuliwa.

Kwa mujibu wa kituo cha Runinga cha Chaneli Ten, kimeeleza kuwa mvua hiyo iliyoanza kunyesha majira ya saa 5 usiku kwa takribani dakika 45 na mpaka sasa mtu mmoja amepoteza maisha huku watu 49 wakijeruhiwa.

Jana Mbunge wa Jimbo la Kwela, Mhe. Aloyce Malocha alifika katika eneo hilo la tukio na kuwafariji wananchi wake na kuwataka watendaji kuangalia namna ya kuwahifadhi wahanga hao kwa muda kabla ya serikali kuangalia namna ya kurejesha miundombinu ya shule na maeneo muhimu yaliyoathirika na mvua hizo.

Jumamosi iliyopita Tamasha la Wasafi Festival, liliahirishwa mkoani humo kufuatia mvua kali iliyonyesha usiku wa siku ya tukio.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents