Soka saa 24!

SUMBAWANGA: Mvua ya ajabu yasababisha Tamasha la Wasafi Festival kusitishwa, WCB watoa kauli

Tamasha la Wasafi limeahirishwa Sumbawanga mpaka kesho (leo) kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mjini hapo. Lavalava alikuwa msanii wa mwisho kupeform kabla ya mvua hiyo kuchapa kwa zaidi ya masaa 2.

Mvua hiyo ilisababisha shoti za umeme uwanjani na baadae muziki na taa kuzima hali ambayo ilipelekea Diamond kupanda stejini na kuwaeleza kwamba show hiyo itarudiwa (kesho) leo jioni.

Kwanza Niwashukuru sana Kwa Mapenzi yenu Mizito juu yetu na #WasafiFestival2018 …..Upendo mliouonesha jana ni Mkubwa sana… na poleni kwa Mvua iliotokea hadi kupelekea mimi na baadhi ya wasanii kutoweza Kuperform….ila kwa kuthamni Sapoti na Upendo wenu juu yetu Leo kuanzia saa sita Kamili Mchana, tutakuwa pale uwanja wa NELSON MANDELA Kuimba na Kucheza na wewe…..Na ikinyesha tunanyesha nayo!!! Mxiiiiiiiiiiiew!!! …Halafu kubwa zaidi HAKUNA KIINGILIO…. YANI KIINGILIO BUUUUUUUUUREEEEEEEEEEEE…!!!!! Njoo na familia nzima baba mama watoto, wote Tukutane Nelson Mandela kuanzia saa sita Mchana SUMBAWANGA!!!

Diamond alisema show hiyo itarudiwa leo saa 10 jioni bila kiingilio ili kukata kiu ya mashabiki hao.

Kwa sasa tamasha hilo linakwenda kufanyika Zanzibar siku ya Jumanne ya wiki ijayo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW