Burudani

Summer Sixteen ya Drake yawa ziara ya hip hop iliyoingiza fedha nyingi zaidi

Drake si rapper wa mchezo mchezo. Mwaka 2016 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwake. Na sasa, ziara yake, Summer Sixteen imekuwa ziara ya hip hop iliyoingiza fedha nyingi zaidi katika historia.

Kwa mujibu wa Pollstar, ziara hiyo ya Drizzy aliyosindikizwa na Future, iliingiza dola milioni 84.3, kwa kuuza zaidi ya tiketi 752,000, ambapo wastani wa tiketi moja ni $112.

Hivyo, Drake ameipiku ziara ya Jay Z na Kanye Westm, Watch the Throne Tour, iliyoingiza dola milioni 75.6 mwaka 2012. Pamoja na hivyo, Summer Sixteen ilikuwa na show 56 tu huku Watch the Throne ikiwa na 63.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents