Supa Pesa Yazidi toa mamilioni

 

Kampuni ya Supa Pesa inayochezesha bahati nasibu kupitia simu za mkononi jana ilitangaza kuongeza zawadi kwa washindi wa bahati nasibu hiyo kwa kipindi kifupi kijacho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Bw. Harm Fourie, alisema kuwa zawadi hizo itakuwa ni pamoja n kuongeza idadi ya washindi  wa kila siku kutoka watatu washindao miloni moja moja mpaka kuwa watano au sita katika  sherehe ya kuwazawadia washindi wa droo za wiki iliyofanyika katika hoteli ya seacliff ambapo wengi kati ya washindi waliopita walikuwepo wakatoa ushuhuda wa ushindi, katika sherehe hizo.

Vilevile msemaji mkuu wa Supa Pesa,Natasha Issa, ameongezea kusema kuwa bahati nasibu hiyo kwa sasa inapata wateja wengi ambapo wametuma meseji mpaka elfu 20 kwa kipindi cha wiki tatu tangu kuanzisha kwa bahati nasibu hii.

‘Droo hiyo inalenga kuwainua kimaisha wananchi hivyo kwa miaka ya baadae kama wakiendelea kuwepo wanaweza kusaidia zaidi hata katika nyanja ya elimu.’ alisema Bi. Issa.

Idadi ya washindi wa milioni moja mpaka sasa ni 36, washindi wa milioni kumi wakiwa wawili na kufanya idadi ya fedha iliyoshindwa kuwa milioni 56.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents