Burudani

Super Soul Sunday: Hatua ya kwanza ni kuamini

Ni jumapili nyingine nakuletea nukuu kutoka kwa watu ambao wamefanya mambo makubwa au ya kipekee katika ulimwengu huu, Nukuu za leo zimelenga kukujengea imani (belief) kuelekea mafanikio yako. 

  1. Ili kufanikiwa ni lazima kuamini kwanza katika yale tunayoyaweza – Michael Korda.
  2. Kile ambacho akili ya mtu inaweza kukipokea na kikiamini, akili (yeye) yake inaweza kukifanikisha – Napoleon Hill.
  3. Ishi katika imani yako na unaweza kuubadili ulimwengu unaokuzunguka –Haenry David Thoreau.
  4. Amini katika kile unachokifanya na sio kile watu wengine wanachosema –Jacob Geit Dekker.
  5. Imani yako itaonyesha matendo yako, na matendo yako yataonyesha matokeo. Lakini cha kwanza ulichokuwa nacho ni imani – Mark Victor Hansen.
  6. Hatu ya kwanza na muhimu kuelekea mafanikio, ni kuhisi au kuamini kuwa tunaweza kufanikiwa – Nelson Boswell.

Shukrani, dondosha comment yako hapo chini kuelezea ni nukuu ipi imekubamba zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents