Burudani

Super Soul Sunday: Vitu saba kuhusu fursa

Kila Jumapili nakusongezea nukuu saba kutoka kwa watu ambao wamefanya mambo makubwa au ya kipekee katika ulimwengu huu. Nukuu za leo zimejikita katika fursa (opportunity), ambapo utajifunza mambo kadhaa kuhusu mada husika.

  1. Katikati ya ugumu wa kila jambo kuna fursa – Albert Einstein.
  2. Hakuna mafanikio ya mbeleni katika kazi yoyote, mafanikio huwa kwa anayemiliki kazi husika – George Crane.
  3. Mtu mwenye busara hutengeneza fursa nyingi kuliko kuzitafuta – Francis Bacon.
  4. Wakati wote fursa zipo kila sehemu, jifunze kuziona na kuzitengeneza – Jacob Geit Dekker.
  5. Inawezakana isitokee fursa ya pili, hivyo ni kujaribu kushikilia ile ya kwanza – Delno L. A. Troup
  6. Fursa au mafanikio hayakufuati wewe… toka ufayafuate – Marva Collins.
  7. Hatuhitaji nguvu zaidi, uwezo zaidi au fursa kubwa. Tunachohitaji ni kutumia kile tulichonacho – Basil S. Walsh.

Shukrani, dondosha comment yako hapo chini kuelezea ni nukuu ipi imekubamba zaidi.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents