Aisee DSTV!

‘Surprises’ zazitawala Tuzo za Watu 2015 (Picha)

Tuzo za watu 2015 zimetolewa Ijumaa hii kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa ‘surprises’ za kutosha. Mshindi mkubwa kwenye usiku huo na ambaye amekuwa surprise kwa wengi ni mtangazaji wa TBC FM, D’jaro Arungu aliyeibuka na tuzo mbili.

IMG_0917
Millard Ayo na Salim Kikeke

D’Jaro alikuwa akishindana na Millard Ayo kwenye vipengele hivyo viwili ambaye hata hivyo alishinda pia kipengele cha blog inayopendwa.

IMG_0770
D’Jaro Arungu akiongea baada ya kutangazwa mshindi

“Mtu yeyote aliyekuwa anashindani halafu anaamini anaweza kupata nafasi lazima imshtue,” Millard ameiambia Bongo5.

IMG_0789
Millard Ayo akipokea tuzo ya blog inayopendwa

“Lakini inakushtua kwa njia nzuri kwamba kuna kitu kimemiss au labda unatakiwa ufanyie kazi zaidi. Lakini pia kura zinamata, inachangia sehemu zote, inawezakana ubora wa kipindi na kura pia. Lakini all in all mimi nampongeza sana D’Jaro Arungu, ameshinda kura zote mbili, ni changamoto pia, inatupa nafasi sisi wenyewe kushindana lakini inasaidia pia kufanya kazi kwenye biashara yetu vizuri.”

Wema Sepetu aliyekuwa ametajwa kuwaniwa vipengele vitatu ameibuka na tuzo moja.

IMG_0818
Wema Sepetu akipokea tuzo yake ya muigizaji wa filamu anayependwa

“I’m Grateful… I’m humbled…. I’m out of words… Ila nawapenda for making this happen…. Shout out to all my fans out there… Na haters pia…. I say it’s a new beginning.”

IMG_0813

“Therez more to this…. I take it as a challenge and a wake up call to give you guys more of what you want me to give,” ameandika Wema kwenye Instagram baada ya ushindi huo,” aliongeza Wema.

IMG_0792
Ray akishukuru baada ya kutangazwa mshindi wa kipengele cha muongozaji wa filamu anayependwa

IMG_0767
Salim Kikeke

IMG_0738
Dada wa Alikiba akipokea tuzo kwa niaba ya kaka yake

IMG_0746

IMG_0730
Lady Jaydee akishukuru baada ya kushinda tuzo ya mwanamuziki wa kike anayependwa

IMG_0712
Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamanzima akimkabidhi tuzo Ommy Dimpoz

IMG_0841
Nancy Sumari akiwapongeza washindi

IMG_0836
Luca Neghesti na Nancy Sumari wakifurahia kilele cha tuzo za watu

IMG_0831
Shangwe kwa washindi

IMG_0832

IMG_0825

IMG_0688
Jacqueline Mengi na Nasreen Karim ni miongoni mwa waliohudhuria

IMG_0686
Joh Makini na Salim Kikeke

IMG_0682
Mtu na binamu yake: Wakazi na Lady Jaydee

IMG_0680

IMG_0672

IMG_0664
Luca na Nancy wakizungumzia tuzo za watu 2015

Hii ni orodha kamili ya washindi

Mtangazaji wa redio anayependwa

D’Jaro Arungu – TBC FM

Kipindi cha redio kinachopendwa

Papaso – TBC FM

Mtangazaji wa runinga anayependwa

Salim Kikeke – BBC Swahili

Kipindi cha runinga kinachopendwa

Mkasi – EATV

Blog/Website inayopendwa

Millardayo.com

Muongozaji wa video anayependwa

Hanscana

Muongozaji wa filamu anayependwa

Vincent ‘Ray’ Kigosi

Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa

Wema Sepetu

Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa

Hemedy PHD

Mwanamuziki wa kike anayependwa

Lady Jaydee

Mwanamuziki wa kiume anayependwa

Alikiba

Filamu inayopendwa

Kigodoro

Video ya muziki inayopendwa

Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz

Related Articles

Check Also

Close
Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW