Mitindo

Swahili Fashion Week 2010

Swahili Fashion Week 2010 Press Conference

Mustafa Hassanali anatuletea Swahili Fashion Week kwa mara ya tatu na mwaka huu itafanyika katika viwanja vya wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Mustafa ambaye ni muaandaaji wa maonyesho hayo leo ameongea na waandishi wa habari katika Hoteli ya Southen Sun na kusema kuwa onyesho la mavazi litaanza kurindima kuanzia tarehe 4 mpaka 6 mwezi wa 11 mwaka huu na liatwashirikisha wabunifu 24 kutoka nchi zinazongea kiswahii ili kuwezesha ubunifu wao wa mavazi ya aina mbalimbali kwa kutumia malighafi tofautitofauti.

 

Wabunifu watakao onyesha mavazi katika Swahili Fashion Week ni pamoja na Aliinda Sawe, Kemi Kalikawe, Manju Msita, Christina Mhando, Farha Naaz Sultan, Gabriel Mollel, Robi Moro, Asia Idarous, Zamda George, Khadija Mwanamboka, Jamila Vera Swai, na Made by Afrika. Wabunifu kutoka Kenya ni Sonu Sharma, Moo Cow, Kikoromeo, John Kavishe na Kikororo na mbunifu kutoka Uganda ni Stella Atal.

Mustafa alisema mwaka huu Swahili Fashion Week itakuwa ya kipeke kwani kutakuwepo pia na maonyesho ya bidhaa mbalimbali za asili, na zenye asili ya mswahili kutoka mwambao wa Afrika Mashariki.

Mustafa alisema “tumeamua kufanya hivi ili kuwapa fursa watazamaji wapya wa Swahili Fashion Week kununua bidhaa mbalimbali na tamasha hili lina bidhaa zinazokwenda na maisha halisi ya jamii ya watu waozungumza lugha ya  Kiswahili”.

Pia aliongezea kuwa tamasha hili litapambwa na burudani ya muziki, wachoraji hina na usukaji mikeka, sambamba na semina za aina tofauti zitakazo washirikisha wabunifu wa mavazi.

Aidha Swahili fashion Week imeandaa aina tofauti za zawadi zitakazotolewa mwaka huu kwa lengo la kutambua na kuthamini vipaji vya aina mbalimbali vitakavyooneshwa, ikiwa ni pamoja na zawadi ya mwaka kwa mbunifu anaechipukia, uchoraji wa hina, usukaji mikeka, sambamba na semina za aina tofauti zitakazo washirikisha wabunifu wa mavazi.

Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na Home of Swahili Fashion week Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, EATV, East Africa Radio, Malaria Haikubaliki, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery Ltd, 1&1 internet solutions, Sengi Tours, Ifashion na 361 Degrees.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents