Mitindo

SWAHILI FASHION WEEK KUONESHA MAVAZI

hassanal_s_office_on_face10th-oct-2011-2

Swahili Fashion Week, Onesho kubwa la mavazi Afrika Mashariki na Kati, imealikwa kuonesha ubunifu wa mavazi yao kwenye  maonesho ya Fashion Business Angola, nalo likiwa onesho kubwa la mavazi Afrika Magharibi nzima likileta pamoja wabunifu zaidi ya 40 kutoka nchi 26 duniani,


Fashion Business Angola itafanyika kuanzia tarehe 14-16 Oktoba mwaka huu,  Filda iliyopo Luanda, na kwa mara ya pili Tanzania tutawakilishwa na wabunifu watatu ambao ni, Manju Msita, Gabriel Mollel and Mustafa Hassanali.

“Mustafa Hassanali  alipata nafasi ya kuonesha mavazi yake mwaka jana kwenye Fashion Business Angola, na kwa mwaka huu wabunifu wawili tena wengine wamepata nafasi ya kuonesha kazi na ubunifu wao hivyo kusaidia kazi hizo kutambulika katika nchi zinazoongea kireno. Ambapo kwa mwaka huu nafasi hii imeenda kwa Manju Msita na Gabriel Mollel wataungana kama timu hasa ukizingatia tunasherehekea miaka 50 ya UHURU.” alisema Enstenium Mgimba, Afia Habari na Mahusiano-SFW

Hassanal_s_office_on_10th-oct-2011-3

Swahili Fashion week kwa sasa ina  programu mbadala na Mozambique Fashion week, FAFA (Festival of Arts and Fashion) iliyopo Kenya vile vile Fashion Business Angola. Wabunifu kama vile Manju Msita, Jamilla Vera Swai and Robi Morro wameshawahi kupata nafasi ya kuonesha kazi zao kwenye maonesho hayo.

“Tunamalengo ya kutangaza biashara ya mitindo katika mataifa mbalili. Ningependa kuwashukuru washirika wetu wote,na wale wote waliotuunga mkono kuanzia miaka ilioyopita na hata sasa.Na pia ningeomba kutoa wito kwa jumuiya na mashirika mbalimbali kutuunga mkono mwaka huu katika maonesho ya mavazi ya wiki ya Swahili.”alisema Afisa habari na mahusiano Enstenium Mgimba

Swahili fashion week 2011 imedhaminiwa na ,the home of Swahili Fashion Week – Southern Sun, EATV, East Africa Radio, Precision Air, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania), Amarula, Ultimate Security, REDD’S original, Image Masters, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Nipashe, Perfect Machinery Ltd, Michuzi blog, PKF Tanzania and 361 Degrees.

Hassanali_One_of_the_invited_Designer_Manju_Msita_explaining_to_the_press_about_the_Showcase_of_Swahili_Fashion_Week_in_Angola_next_is_the_PRO_of_Swahili_Fashion_Week_and_designer_Gabriel_Mollel_on_10th-oct-2011-1

KUHUSU SWAHILI FASHION WEEK

Swahili fashion week ni jukwaa la wabunifu wote katika mavazi na vito kutoka katika nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili na kuonesha ubunifu wao, kutangaza sanaa zao ili kupata wateja wa bidhaa zao. Hii yote imelenga katika kukuza sanaa ya maonyesho ya mavazi na kujipatia kipato, kutengeneza ajira ili kuhamasisha katika lengo la kuwa na (Bidhaa kutoka Afrika Mashariki)

Swahili Fashion Week ni maonyesho makubwa yatakayohusisha Afrika mashariki na kati, . Kwa mwaka wake wa nne sasa Swahili Fashion Week itasheherekea miaka 50 ya Uhuru kwa kuleata pamoja wabunifu 50 kutoka Tanzania,nchi za jirani na duniani kote katika kusheherekea siku yake ya UHURU

Kwa kuanzisha kitu cha tofauti na chenye kuleta matumani katika ubunifu wa jukwaa la maonesho ya mavazi, Swahili fashion week imekua moja ya tamasha kubwa la maonesho ya mavazi kwa ukanda wa Afrika na soko la kimataifa, mtazamo wa 2008 kutoka kwa Mustafa Hassanali.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents