Bongo Movie

Swali la Jaji kwa Lulu, ‘Kipindi unaendesha gari ulikuwa na leseni halali?'(+Picha)

Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili muigizaji, Elizabeth Michael (Lulu) imeendelea Mahakama Kuu ya Tanzania, ambapo leo muigizaji huyo alipata nafasi ya kujitetea katika Mahakama hiyo. Lulu ameeleza A-Z walivyokuwa na mahusiano na Marehemu Steven Kanumba hadi umauti ulivyomkuta msanii huyo.

Jaji Sam Rumanyika alimuuliza maswali Lulu kama ifutavyo:

Jaji Sam Rumanyika?: Kipindi unaendesha gari ulikuwa na leseni halali?

Lulu: Hapana.

Jaji Rumanyika?: Leseni ulipata lini.

Lulu: Sikumbuki vizuri

Hata hivyo Lulu alivyoulizwa kuhusika na kifo cha Kanumba kwa namna yoyote ile amesema “Kwa namna yoyote ile mimi sijasababisha kifo cha Kanumba, na mimi ndiye nilieshambuliwa na marehemu kutokana na umbile langu nilikuwa mdogo na alikuwa na uwezo wa kufanya chochote kwenye mwili wangu kwasababu yeye ndo alikuwa na silaha.”


Lulu akisalimiana na msanii mwenzie wa filamu, Dkt Chein aliyekuwepo Mahakamani hapo.

Mrembo huyo wa filamu anakabiliwa na kesi ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba tukio linalodaiwa kufanyika mwezi Aprili mwaka 2012.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents