Michezo

Swansea City yamtimua kocha wao Garry Monk

Klabu ya Swensea City hatimaye imemtimua kocha wake Garry Monk baada ya kushinda mchezo mmoja kati ya 11 ambayo ameingoza Swansea kwenye ligi ya England msimu huu.

2F2C01D600000578-3353199-image-a-5_1449698720082

Kocha huyo mwenye miaka 36 ameitumikia klabu hiyo zaidi ya miaka 11 akianza kama mchezaji lakini baadaye mwaka 2014 akakabidhiwa timu hiyo kama kocha mkuu akichukua nafasi ya Michael Laudrup.

Kufuatia kipigo cha Jumamosi iliyopita cha magoli 3-0 dhidi ya Leicester City ulikuwa ndio mchezo wake wa mwisho kama kocha na ameiacha timu hiyo katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi.

Kocha huyo alijiunga na Swansea City kama mchezaji mwezi June mwaka 2004, akaisaidia Swansea kupanda daraja kucheza ligi kuu mwaka 2011 akiwa nahodha wa timu hiyo.

February 2014 aliteuliwa kuwa kocha wa muda lakini May 2014 akapewa nafasi hiyo kama kocha mkuu.

Mwezi August 2014 Swansea ilipata ushindi wa ugenini dhidi ya Manchester United na huo ukawa ni ushindi wa kwanza kwa Swansea kwenye uwanja wa Old Trafford.

Swansea ilimaliza katika nafasi ya juu kwenye ligi msimu wa 2014-15 ikiwa nafasi ya nane kwa kufikisha jumla ya ponti 58.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents