Michezo

Sweden yasonga mbele kibabe kombe la dunia, yaipa mkono wa kwaheri Ujerumani

Timu ya taifa ya Sweden imefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia baada ya kumfunga aliyekuwa kinara wa kundi hilo Mexico kwa jumla ya mabao 3 – 0.

Mabao ya Augustinsson dakika ya 50, Granqvist dakika ya 62 na Álvarez 74 yalitosha kuwahakikishia nafasi hiyo na kupindua msimamo wa kundi hilo na kuwa vinara kwa tofauti ya magoli dhidi ya Mexico.

Kwenye lindi hilo la F, bingwa mtetezi timu ya taifa ya Ujerumani inaungana na Korea Kusini kuyaaga mashindano hayo baada ya mchezo wao kumalizika kwa matokeo ya Ujerumani kufungwa 2 – 0.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents