Sweta la 50 Cent lazua tafrani!!

Umati mkubwa wa watanzania ulionekana kwa wingi katika maeneo ya uwanja wa ndege wa zamani siku ya jumamosi kwa ajili ya kumpokea msanii mkubwa na maarufu duniani Curtis Jackson a.k.a 50 Cent ambaye alitua majira ya saa tisa alasiri

Watu wakimsubiri 50 Cent


 


[Bofya hapa kuangalia video za 50 Cent alipofika uwanja wa ndege]


 


Umati mkubwa wa watanzania ulionekana kwa wingi katika maeneo ya uwanja wa ndege wa zamani siku ya jumamosi kwa ajili ya kumpokea msanii mkubwa na maarufu duniani Curtis Jackson a.k.a 50 Cent ambaye alitua majira ya saa tisa alasiri kiwanjani hapo na kulakiwa n maelfu ya mashabiki.



50 Cent ambaye alikuwa akitokea nchini Afrika Kusini alikokuwa na onesho, aliambatana na machizi wake wa G-Unit akiwemo Tonny Yayo na Lloyd Banks pamoja na timu kubwa ya watu kadhaa ambao walikuwa katika harakati za kuhakikisha watanzania wanapata kile ambacho mtu mzima huyo aliwaandalia.



Licha ya kuwepo Mashabiki pia wadau mbali mbali mbali mbali wa burudani nchini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Clouds FM Mr Joseph Kusaga, Kinje pamoja na na Meneja masoko wa kampuni ya Tigo Kevin Twissa wote walikuwa mstari wa mbele katika kumpokea mkali huyo.



Mshikemshike wa aina yake ulizuka mara tu Mnyamwezi 50 Cent alipojitekeza nje ya uwanja wa ndege wa zamani wa hapa nchini, alisababisha tafrani kubwa sana iliyopelekea baadhi ya mashabiki kuumia pale alipotupa sweta lake kwa mashabiki, almanusra watu watoeni macho mpka kufikia hatu ya polisi kuingilia kati juhudi ambazo hazikuzaa matunda yoyote.


 


Watu wakigombania sweater
Bofya picha kuangalia video ya kitimtim hicho


 



Mpaka tunatondoka eneo la tukio suluhu haikuwa imepatikana baina ya mashabiki hao kuwa nani achukue sweta hilo?



Watu wakigombania sweater


 


Msafara mkubwa alioongozwa na vijana watano walio nadhifu na wakakamavu ambao walikuwa ndani ya suti nyeusi huku kila mmoja akiendesha gari aina ya Mercederce Benz nyeusi ambazo zilijipanga kwa kufuatana katika mapokezi hayo.



Unaweza kusema kulizuka vurugu lakini hazikuwa vurugu bali ni furaha iliyopitiliza kwani kila mtanzania alionekana kudata baada ya mnyamwezi huyo kuchomoka ambapo kila aliyekuwa mbali alitaka kumkaribia na kumshika lakini mchizi alisepa na kuzama ndani ya gari aina Range Rover ambayo ilikuwa maalum kwa ajili yake na kuelekea Kempinsiki Kilimanjaro Hotel kwa ajili ya mapumziko na kuzungumza na waandishi wa habari.


 


50 Cent akiwa na Joseph Kusaga katika press conference
50 Cent akizunguumza na waandishi


 


50 Cent akisalimiana na Kelvin Twissa
50 Cent akisalimiana na meneja masoko wa kampuni ya Tigo Kelvin Twissa


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents