Aisee DSTV!
SwahiliFix

Sylivia Sebastian ashindwa kuamini baada ya kutangazwa mshindi Miss Tanzania 2019, aona kama ndoto (+Video)

Hapo jana siku ya Ijumaa Agosti 23 mwaka huu wa 2019, Tanzania imeweza kupata mrembo mpya kupitia mashindano ya Miss Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam, ambapo wadau wa tasnia ya urembo iliweza kushuhudia mwanadada kutoka mkoani Mwanza, Sylivia Sebastian akitwaa taji hilo na kutarajiwa kuliwakilisha taifa huko duniani. Baada ya kutangazwa kuwa yeye ndiye mshindi wa taji hilo la Miss Tanzania 2019, Sylivia Sebastian ameonekana kama kutoamini matokeo hayo na kushikwa na bumbuwazi kwa dakika kadhaa jukwaani huku katika mahojiano na vyombo vya habari akisema kuwa hakutarajia kuwa angetawazwa kuwa mshindi kwa usiku huo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW