DStv Inogilee!

Sylvester Stallone aridhia filamu ya Rambo iigwe Bollywood

Kupokea ujumbe kutoka kwa Sylvester Stallone kuhusu kuigwa upya filamu ya Rambo kihindi ni kama “kuungwa mkono na Mungu”, mkurugenzi wa filamu hiyo amesema.
Sid Anand amewambia mashabiki filamu hiyo haitokuwa na nyimbo na kucheza dansi kama ilivyozoeleka kwa filamu za Bollywood .

“Siwezi kuifanya hivyo Rambo,” ameiambia BBC. “Itakuwa ni kama kumkosea Mungu.”
Filamu hiyo inazinduliwa katika maonyesho ya filamu ya Cannes – Hatahivyo filamu yenyewe itaanza kurekodiwa baadaye mwaka huu.

Muigizaji nyota wa India, Tiger Shroff, ndiye anae lipokea jukumu hilo kuu.
Kuhusu uamuzi wake wa kuizindua filamu hiyo Cannes, Anand amesema: “Rambo anatambulika katika kila sehemu ya duniani. Kwahivyo ni muhimu kuizindua filamu hiyo katika eneo kuu la utengenezaji Filamu.”

Amesema amepata msukumo wa kuitengeneza filamu hiyo Kihindi kutokana na uzito wa muigizaji mkuu “muigizaji wa kweli wa kupigana aliye na moyo mkubwa”, aliyefufuliwa na Stallone.

Anand amesema ameipangilia filamu hiyo kwa namna ambavyo itakuwa rahisi “kueleweka India” – lakini ameonya: ” Huenda ikazusha mzozo kama ilivyokuwa kwa Rambo First Blood katika miaka ya 80.

“Inakufanya ufikirie, na inhusu hali inayojiri India na inakuwa tofuati kwa namna hiyo.”

Stallone alituma ujumbe katika mtandao wa kijamii wiki iliyopita akisema Rambo ni “mtu sifika”, akiongeza : “Nataraji hawato iharibu.”
Lakini baadaye alituma ujumbe kwa Shroff mwenyewe akimtakia kila la kheri.
“Ameonyesha imani kwa kutuma ujumbe kwenye Twitter. Ni kama “kuungwa mkono na Mungu mwenyewe,” amesema Anand.

Alipoulizwa wanavyofikiria mashabiki wa filamu asili , alisema: ” Nafahamu sio mashabiki wote wa Rambo watakadhibishwa kwa sababu hawataki iharibiwe. Lazima nionyeshe thamani ya maana ya Rambo.
“Filamu aina hizo haizigwi tena, kwahivyo ilinifurahisha kuwaletea vijana wazo hilo.”

Shroff, mwenye miaka 27, amesema anahishi mpango huo ni mzuri sana kiasi cha kutoamini alipofuatwa mara ya kwanza kuarifiwa kuuhusu filamu hiyo.

Alisema: “machini mwangu, Sylvester Stallone atasalia kuwa Rambo. NI shujaa wangu.

“Sitaki kuchukuwa mahala pake lakini kutoa mtazamo tofuati kuuhusu. “Ni jukumu kubwa kujitwika.”
Filamu hiyo inaanza kuigizwa mwishoni mwa mwaka katika milima ya Himalayas na itatoka rasmi mwaka 2018.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW