Michezo

Syria yazima ndoto za China kombe la Dunia

Timu ya Taifa ya Syria imeweka hai matumaini ya kushiriki kwa mara ya kwanza michuano ya Kombe la Dunia baada ya kutoka sare dhidi ya China katika mchezo uliochezwa siku ya Jumanne.

Mchezaji wa timu ya Syria (mwenye jezi nyekundu) akikabiliana na mchezaji wa timu ya Taifa ya China

Mchezaji Ahmad Al Salih, alikuwa mwiba mkali mbele ya China baada ya kuisawazishia timu yake katika dakika za lala salama na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya magoli 2 kwa 2.

Syria inashika nafasi ya nne katika kundi lao, ikiwa na alama tatu nyuma ya timu ya taifa ya Uzbekistan ambao wana michezo miwili mkononi huku timu ya taifa ya Iran ikishika nafasi ya kwanza.

Wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka wa 2022, Qatar, iliishangaza Korea Kusini kwa ushindi wao wa magoli 3-2, katika kundi hilo zinahitajika timu mbili ili kuweza kujikatia tiketi ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Timu ya taifa ya China inayo nolewa na Meneja, Marcello Lippi inaburuza mkia katika kundi hilo la A.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents