Michezo

Taarifa kwa umma kutoka Yanga

Klabu ya soka ya Yanga inapenda kuwatangazia wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau wa soka jijini Dar es salaam sanjari na mikoa ya karibu kwamba; mchezo wa Jumamosi kati ya Yanga SC na Mbeya City utachezwa uwanja mkuu wa taifa kuanza saa 10:30 kama ilivyo ada.

Maamuzi haya yamezingatia matakwa na masilahi ya wadau wa soka nchini ambao wana kiu na hamu ya kuutazama mchezo huo lakini pia wakiwa ni sehemu ya wadau wa mchezo wa riadha itakayofanyika uwanja wa taifa jumamosi hiyo hiyo.

Tunawaomba wanachama na mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa sapoti vijana wao.

Nyote mnakaribishwa

Imetolewa na Idara ya habari na mawasiliano
Young Africans Sports Club

12.05.2017

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents