Habari

Taarifa ya CHADEMA kuhusu hali ya afya ya Mbunge Halima Mdee

Mbunge wa Kawe jijini Dar es salaam kupitia CHADEMA Halima James Mdee, amelazwa katika hospitali ya Agakhan jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu.

Taarifa zilizothibitishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi na uenezi wa CHADEMA, John Mrema amesema kwamba Halima Mdee amefanyiwa upasuaji wa kutolewa uvimbe aliokuwa nao tumboni.

“Amefanyiwa upasuaji alikuwa na uvimbe tumboni. ..yuko Agakhan”, amesema John Mrema.

Hii leo baadhi ya Wabunge wametoa ujumbe wao wa pole kumtakia Mbunge huyo kupona kwa haraka, ili aweze kurejea kwenye majukumu yake ya kawaida.

https://www.instagram.com/p/BycPXeAl770/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents