Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Michezo

Taarifa ya Send off ya Zabaleta Manchester City

By  | 

Klabu ya Manchester City imepanda hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya ushindi mnono wa magoli 3 kwa 1 uliopatikana dhidi ya klabu ya West Brom, mchezo uliochezwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad Stadium.


Manchester City 3-1 West Brom

Na hii niripoti kamili

Magoli ya Gabriel Jesus, Kevin De Bruyne pamoja na Yaya Toure yaliifanya timu hiyo kutoka kifua geni katika uwanja wa nyumbani.

West Brom walionekana wakiwa nje ya mchezo na kurejea mchezoni katika dakika za lala kwa buriani kufuatia mabadiliko ya kuingia mchezaji Hal Robson-Kanu.

Kwa matokeo hayo, City inaingia katika nafasi ya nne za juu, lakini kwa matokeo ya klabu ya Arsenal dhdi ya Sunderland inaacha vita kubwa kati ya klabu hii ya the Gunners na mojogoo wa Landani klabu ya Liverpool ili kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Pamoja na hayo, City imejihakikishia kushiriki mashindano hayo ikiwa ina kibarua kigumu dhidi ya Watford siku ya Jumapili.

Kutakuwa na kibarua kigumu kwa mlinzi wa City, Zabaleta, ambaye alitangaza kuondoka ndani ya klabu hiyo, pamoja na Mchezaji, Toure, ambaye pia ataondoka.
Ilichukua dakika 13 pekee kudhihirisha kuwa wapo kikazi zaidi baada ya mchezaji, Aleksandar Kolarov’s kufunga goli ililotokana na mpira wa free-kick wa Ben Foster.
Baada ya mchezo huo Mchezaji wa Manchester City Pablo Zabaleta alikiambia chombo cha habari cha Sky Sports:


Send off ‘will stay with me forever’ – Zabaleta

” Mara ya kwanza kuja Manchester sikufikiria kama nitaweza kukaa kwa kipindi kirefu. Kuwa hapa katika siku ile ya kwanza kulinifanya nijivunie sana”.
“Katika maisha ni lazima wakati mwingine ukubali kuchukua maamuzi magumu na hivyo siku zote ninaona ni kama njia sahihi kwangu, kwa familia yangu na klabu yangu kwa ujumla”. Nafikiria sasa ni muda sahihi wa mimi kuendelea na mambo mengine lakini niamini”. Naipenda sana hii klabu ”.

“Asante kwa mashabiki, na kila mtu… kwa sababu mmenifanya mimi niwe mchezaji mzuri na mtu mzuri na siku zote nitaiombea mema.


Mlinzi wa Manchester City Pablo Zabaleta

“Ilikuwa vigumu sana kucheza dakika zote 90. Kwakuwa nilijawa na hisia mno, na kumbukumbu zote hizi zitasalia katika kichwa changu lakini kama nilivyoweza kusema mwanzo, najivunia sana katika hili. Kwa kile nilicho kifanya hapa katika klabu ndio kitu ambacho kila mchezaji anapaswa kufanya katika timu anayo ichezea.


Mashabiki wa klabu ya City wakimpongeza

“Najivunia kuwa sehemu ya historia ya mafanikio ya klabu hii ya City’, ahsanteni sana.”

Alipoulizwa ni kipindi kipi alifurahia zaidi kuwa City akajibu, Zabaleta : ” Kwa mara ya kwanza tulivyoweza kumfunga Manchester United katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA katika Uwanja wa Wembley mwaka 2011, na katika mchezo wa kwanza wa ligi tulivyo shinda , goli la (Sergio) Aguero’s .


Akitoa shukurani lupitia mtandao wa Twitter

“Na Msimu wa pili wa ligi tulivyo kuwa na Kocha ,Manuel Pellegrini, goli langu la ugenini dhidi ya klabu ya Rome katika mashindano ya klabu bingwa, Nina kumbukumbu nyingi nzuri siwezi kuzikumbuka zote”.

“Nilikuwa na bahati sana kucheza karibu na wachezaji bora hakika ni swala la kujivunia.
“Nitafurahia uwepo wangu wa kuwa hapa katika kipindi hiki kifupi kilicho baki na tumebakiwa na mchezo mmoja. Nikuwa bora katika klabu hii” Alisema Zabaleta.

BY HAMZA FUMO

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW