Michezo

Taarifa ya Simba SC kufungwa goli 6-0 nchini Uturuki yazua gumzo, Manara awataka Clouds FM waombe radhi

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amekiomba kituo cha Radio cha Clouds FM kuomba radhi kwa mashabiki wa klabu hiyo kwa kutangaza kuwa wamefungwa goli 6-0 nchini Uturuki kwenye mchezo wa kirafiki.

Haji Manara

Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa kama kituo hicho kitakataa kuomba radhi basi kithibitishe taarifa hizo kwani inaonekana ni ya uongo na inachafua brand ya Simba.

Ndugu zangu wa Clouds with do respect mnachotufanyia c haki na mnatukosea sana tena sana!! Leo mmetangaza kwenye Radio yenu Simba imecheza mechi Uturuki na kufungwa 6-0..tunaomba mthibitishe au mkanushe..vinginevyo mtakuwa na nia ovu ya kutudhalilisha na kwa hili hatutawaelewa na hatutakubali!! Mm wajibu wangu pia ni kulinda image ya Club yangu na sipo tayari kuona Chombo chochote kikitangaza taarifa ya uzushi na uongo dhidi ya Simba kwa kisingizio chochote kile..kwa hili nategemea mtachukua hatua stahiki haraka iwezekanavyo .vinginevyo thibitisheni @cloudstv @cloudsfmtz

Hata hivyo, mpaka sasa Clouds Media hawajaomba radhi wala kuthibitisha taarifa hizo kama ni za kweli au laah!.

Klabu ya Simba imeondoka wikiendi iliyopita kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2018/19 na ikiwa huko imeelezwa kuwa itacheza michezo kadhaa ya kirafiki.

Related Articles

34 Comments

  1. Me menyew nipo Simba tusipende kupokea taarifa za ushindi tuu ni lazima tukubaliane na matokeo ya aina yyte,maana cloudz wametutajia mpk wafungaji,pengine huyu jamaa yetu anataka tu kupindishapindisha ukweli ili kukwepa aibu ya kufungwa,mie cjakurupuka Kama unavyodhani,ila naww inabidi utumie akili yko badala tu ya kushadadia ushabiki wa kizamani wa usimba na uyanga

  2. Kabisa hawa clouds nimewasikia asubuhi PJ alisema kwenye kipindi cha break fast
    Waache kutoa habari zisizokuwa na uhakika kama ikibaika ni uwongo wachukuliwe hatua zaidi kwani miiko ya utangazaji sio kutoa habari zisizo na uhakika

  3. Inatakiwa ujiongeze Na wewe , mbona vyombo vingine vyote vya habari hawajatangaza hyo taarifa ? Inamaana hao clouds ndo wanapata taarifa wenyewe?, Na kutaka wachezaji CO shida kwan kama unawajua wachezaji wa timu husika kwann usitaje Kwa kuwaaminisha watu ,hata hivo hyo timu c ya uturuki n ya swazland Na inashiriki lig kuu huko, ofcoz hao clouds wapo kishabiki Na naomba uongoz wa simba wachukue hatua Kali za kisheria zid yao ,hizo n taarifa za kichochezi

  4. haahahhahahahhahhahahhaahhahahahhahahahahahhahahahahhahahhhahahahahhahahahahahahhahaahahahhahahahahhahahahahahahahhhahhhhhhhhaahahahahhahahahahahhaahahahkumamaehahahahahahhahhahahahhahhaaaaaah

  5. Sio lazima vyombo vyote vya habari vitangaze Luka hii inategemea na ufuatiliaji wa habari pengine inawezekana cloudz wana watu wao kule ambao wameleta habar najua mngeambiwa Simba kashinda msingehoji chochote,ila kwa kuwa tumepigwa cha mbwa Koko ndo mana naona mnahoji hoji hili halihitaji kujiongeza wala Nini zaidi ya kupokea taarifa ya kipigo,pia lazima utambue bora ukapigwa mapema ili utambue udhaifu wako upo maeneo gn ili ujipange kuliko kuchagua tim mbovu ukaifunga afu ukajidanganya kua una Tim nzr tukumbuke hizi ni friend match

  6. Chidy nimekuelewa vzr watu wanasahau kuwa mpira wa uturuki upo juu kuliko sisi tunapenda kulazmisha kua Simba haiwez kupigwa goli nyingi na waturuki wkt wenzetu washatuacha mbali sn,mpira una matokeo matatu ni lazma kuyakubali yote

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents