Habari

Taarifa za mvua kubwa kutoka mamlaka ya hali ya hewa (TMA)

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa tahadhari kwa umma kuhusu vipindi vya mvua kubwa vinavyoambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa katika mwambao wa ukanda wa pwani.

TMA katika taarifa yake imetoa tahadhari kuwa, kuanzia leo hadi kesho kutwa kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 vinavyoambatana na upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili.

Mamlaka hiyo imesema maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara. Pia, visiwa vya Unguja na Pemba.

“Hali hii inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua nchini na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika Bahari ya Hindi eneo la kisiwa cha Madagascar, hivyo kusababisha upepo mkali katika pwani ya Tanzania,” imesema taarifa hiyo.

TMA imewataka wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari na hatua stahiki.

Soma taarifa kamili:

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents