Habari

Taarifa za TMA: Kimbunga ‘Belna’ chazidi kuimarika 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa mrejeo wa taarifa iliyotolewa tarehe 06 Disemba 2019 kuhusu uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa, ulioendelea kuimarika kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar na kufikia kiwango cha kuwa kimbunga ‘Belna’.

KIMBUNGA BELNA KUSINI MAGHARIBI MWA BAHARI YA HINDI

Kimbunga ‘Belna’ kilichopo kusini magharibi mwa bahari ya Hindi (karibu na kisiwa cha Madagascar) kimeendelea kuimarika hali iliyopelekea kuongezeka kwa vipindi vya mvua katika maeneo machache hapa nchini.

Hata hivyo, kimbunga ‘Belna’ kinatarajiwa kuingia nchini Madagascar mnamo tarehe 10/12/2019, na hivyo kutokuwa na madhara katika nchi yetu. Hii ni taarifa ya mwisho kuhusiana na kimbunga ‘Belna’

Aidha, msimu wa mvua unaendelea katika maeneo mengi nchini (yale yanayopata msimu mmoja wa mvua pamoja na yale yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka), hivyo vipindi vya mvua vinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi nchini. Hali kadhalika, vipindi vya joto vinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi nchini hususan katika nyakati zenye upungufu wa mvua.

USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia utabiri wa saa 24, siku 10, mwezi mmoja pamoja na tahadhari kila zinapotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents