Michezo

Taarifa za usajili barani Ulaya Alhamisi hii, Rashford, Hazard, Ozil, Giroud, Batshuayi, Nani na wengine sokoni

Real Madrid wanaandaa kitita cha pauni milioni 100 ili kumsajili mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 21, kabla hajasaini mkataba mpya na Manchester United mwishoni mwa msimu. (Sun). Kocha Chelsea bMaurizio Sarri amesema kiungo wa Ubelgiji Eden Hazard, 28, anaweza kuondoka Chelsea kama atataka mwishoni mwa msimu.. (Sky Sports)

Paris St-Germain wametoa ofay a dakika za mwisho ya kutaka kumsajili kwa mkopo mchezaji wa Arsenal, Mjerumani Mesut Ozil, 30. (Metro)

PSG pia wanataka kumsajili winga wa Chelsea na Brazil Willian, 30, kwa mkopo kama mbadala wa Neymar ambaye ni majeruhi. (Mail)

West Ham wamefanya mazungumzo na Chelsea wakitaka kujua uwezekano wa kumsajili streka wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, 32. (Mail)

West Ham pia wanamuwinda kiungo wa Chelsea Danny Drinkwater, 28, ili wamsajili kwa mkopo. (Talksport)

Everton wanataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi, ambaye amechezea raundi ya kwanza ya msimu kwa mkopo klabu ya Valencia ya Uhispania. (Guardian)

Klabu ya West Ham pia inamtaka Batshuayi ambaye ni mtaia wa Ubelgiji, akini kwa mkopo. (Sky Sports)

Winga wa zamani wa klabu ya Manchester United Nani, 32, ambaye kwa sasa anakipiga na klabu ya Sporting Lisbon, anatazamiwa kujiunga na ligi ya soka Marekani, MLS. (beIN Sport USA, via ESPN)

West Ham wamekataa kitita cha pauni milioni 7 kutoka Valencia kwa usajili wa mshambuliaji wa Mexico Javier Hernandez, 30. (Sky Sports)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents