Michezo

Taarifa za usajili barani Ulaya Ijumaa hii, Rashford, Ginter, Kante, Mourinho, Coutinho, Grimaldo, Rugani na wengine sokoni

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21, yupo katika mazungumzo ya kina kuhusu kuimarisha mkataba wake ambao huenda ikachangia kuongezwa kwa mshahara wake kwa zaidi ya mara mbili na mkubaliano ya thamani ya £200,000 kwa wiki katika mkataba wa muda mrefu(Star)

Tottenham na Arsenal wanamuangalia beki wa kati wa Borussia Monchengladbach kutoka Ujerumani Matthias Ginter, mwenye umri wa miaka 25. (Sky Sports)

Huenda Paris St-Germain ikatafuta kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea N’Golo Kante, mwenye umri wa miaka 27, katika msimu w a joto. (Le10 Sport, kupitia Sun)

Aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United, Joe Mourinho anatarajiwa kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa Inter, Beppe Marotta kuhusu kuchukua usukani katika klabu hiyo ya Italia kwa mara ya pili. (Mirror)

Huenda Paris St-Germain ikatafuta kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea N’Golo Kante

Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Philippe Coutinho inaarifiwa ‘amehuzunishwa’ kuwepo Barcelona, lakini anaendelea kupata usaidizi kutoka kwa wachezaji wenzake na meneja wake. Manchester United na Chelsea zinafikiria kumfukuzia mchezjai huyo wa miaka 26 katika msimu wa joto. (Sport, kupitia Metro)

Arsenal inaongoza katika kumfukuzia mlinzi wa Benfica Alex Grimaldo, mwenye umri wa miaka 23. Manchester City, Napoli na Inter Milan zote zimehusishwa na beki huyo wa kushoto. (Mundo Deportivo, kupitia Express)

Mchezaji aliyelengwa na Chelsea, Daniele Rugani, mwenye umri wa miaka 24 mchezaji wa timu ya taifa ya Italia anatarajiwa kupokea mkataba ulioimarika huko Juventus hadi 2023. (Calciomercato)

Manchester United bado ina hamu ya kumsajili mchezaji wa Napoli, Kalidou Koulibaly, mwenye umri wa miaka 27, Milan Skriniar, mwenye umri wa miaka 23, wa Inter na pia ina hamu ya kumsajili mlinzi wa tatu, Joachim Andersen, mwenye miaka 22 wa Sampdoria. (Manchester Evening News)

Ander Herrera ana hamu ya kusalia Manchester United wakati majadiliano kuhusu mkataba mpya wa mchezaji huyo mwenye miaka 29 yakiendelea. (Independent)

Chelsea imetuma waangalizi kuwakagua wachezaji watatu wa Ureno Joao Felix, Ruben Dias na Bruno Fernandes katika mpambano wa Derby ya Lisbon. Mchezaji wa kiungo cha kati Felix, mwenye miaka 19, na mlinzi Dias, wa miaka 21, wanaichezea Benfica, huku mchezaji wa kiungo cha kati Fernandes, 24, akiwa upande wa Sporting Lisbon. (O Jogo, kupitia Metro)

Aliyekuwa mlinzi wa Juventus Mehdi Benatia, wa miaka 31, anasema aliamua kujiunga na timu ya Qatar, Al Duhail dhidi ya Manchester United kwasababu anataka kuilea familia yake katika nchi ya kiislamu. (Goal)

Meneja wa Fulham Claudio Ranieri anaamini kaimu meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anastahili kupewa kazi ya kudumu

Meneja wa Fulham Claudio Ranieri anaamini kaimu meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anastahili kupewa mkataba wa kudumu. (Star)

Aliyekuwa Kapteni wa Chelsea John Terry “anatarajia” mchezaji wa kiungo cha mbele Eden Hazard, mwenye miaka 28, atasalia Stamford Bridge. (Talksport)

Bosi wa Brighton Chris Hughton anataka mashabiki wanaowanyanyasa wachezaji soka waadhibiwe ” kwa uzito mkubwa”. (argus)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents