Michezo

Taarifa za usajili barani Ulaya Jumamosi hii, Hazard, De Gea, Rice, Under, Herrera, Hastie, Ndombele na wengine sokoni

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri, amesema hatakuwa kizingiti kwa Eden Hazard ikiwa nyota huyo wa miaka 28 ataamua kujiunga na miamba wa ujispania Real Madrid msimu ujao. (Star). Lakini Cesc Fabregas anaamini Hazard huenda akasaini mkataba mwingine na Chelsea katika hatua ambayo itakomesha tetesi kuhusu uhamisho wako. (Independent)

Tottenham wanajiandaa kuweka dau la pauni milioni 35 kumnunua kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 20, licha ya kukabiliwa na ushindani kutoka kwa mahasimu wao katika ligi ya Uingereza, Liverpool. (Daily Express)

Manchester Unitedwanatarajiwa kuminyana na mahacimu wao Manchester City kumsaini kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele, 22 msimu ujao. (Mirror)


Tanguy Ndombele (kushoto) aliisaidia Lyon kushinda Manchester City katika ligi ya mabingwa mwezi uliyopita

Vilabu vya Chelsea, Manchester United na Liverpool vinapania kumnunua nyota wa Benfica Joao Felix, 19. (TalksporM

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amepuuzilia mbali tetesi kuwa klabu hiyo itatumia fedha nyingi msimu ujao kuwasajili wachezaji wapya. (Teamtalk)

Kipa David de Gea, 28, anakaribia kutia saini kandarasi ya miaka mitano na klabu ya Manchester United. (Metro)

Mchezaji Adrien Tameze, 25,amesema kuwa alikataa kujiunga na Cardiff City au Watford kwasababu anataka kuendelea kucheza chini ya meneja wa Nice Patrick Vieira. (Sport WitnessJ

Matumaini ya Tottenham kuhamia uwanja wao mpya wa White Hart Lane msimu huu yamedidimia baada ya maneja wao Mauricio Pochettino ni vigumu kwao kuhamia uwanja huo kufikia mwezi Mei mwaka huu. (Guardian

Wasimamizi wa Ligi ya Primia wanataka Tottenham kucheza angalau mechi tano katika uwanja wa mpya msimu huu la sivyo waendelee kucheza katik uwanja wa Wembley hadi mwisho wa msimu huu. (Standard

Bayern Munich wanajiandaa kuweka dau la kumnunua,Nicolas Pepe anayechezea klabu ya Lille.

Mchezaji huyo pia anang’ang’aniwa na Arsenal, Manchester City na Barcelona. (Le 10 Sport, via Metro)

Tottenham, Inter Milan na AC Milan wanafuatilia mchezo wa kiungo wa kari wa Porto Hector Herrera, 28. (Calcio Mercato)M

Winga wa zamani wa West Ham, Luis Boa Morte amefichua kuwa hakutaka kuhamia klabu hiyo. (Mais Futebol, via Sport Witness)

Manchester United walipoteza nafasi ya kumsaini beki wa kati wa Red Bull Leipzig Dayot Upamecano baada ya kubadilisha masharti ya ofa yao. (Metro)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents