Michezo

Taarifa za usajili barani Ulaya Jumanne hii, Salah, Sarri, Lampard, Foyth, Rabiot na wengine sokoni

Juventus wanajipanga kutoa kitita cha pauni milioni 175 ili kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah, 26. (Sky Arabia – via 90min) Mustakabali wa Maurizio Sarri kama kocha wa Chelsea utaamuliwa ndani ya wiki mbili zijazo. (Telegraph)

Wachezaji wa Chelsea walifanya kikao maalum cha ‘kurekebishana’ katika uwana wao wa mazoezi wa Cobham jana Jumatatu kufuatia kipigo walichopata cha 6-0 dhidi ya Manchester City. (Mail)

Kocha wa Derby Frank Lampard amepuuzia uvumi kuwa huenda akarithi mikoba ya Maurizio Sarri endapo Chelsea itaamua kumfukuza. (Evening Standard). Beki wa Tottenham Juan Foyth, 21, amefichua kuwa alikataa kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain tili ajiunge na Spurs mwaka 2017. (Goal)

Kocha wa Chelsea raia wa Italia Maurizio Sarri amekalia kuti kavu baada ya mfululizo wa vipigo kwa timu yake.

Barcelona wamefikia makubaliano na klabu ya Eintracht Frankfurt kumsajili streka wao raia wa Serbia Luka Jovic, 21, mwishoni mwa msimu. (Diario Sport). Mshambuliaji wa Juventus raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, anakaribia kufikia makubaliano ya kuhamia Real Madrid mwishoni mwa msimu. (AS)

kiungo wa Paris Saint-Germain Adrien Rabiot, 23, amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa na sasa Man United wameingia kwenye mbio za kumsajili

anchester United wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain Adrien Rabiot, 23,mwishoni mwa msimu. (AS – via Mirror)

Barcelona walitaka kumsajili beki wa kati wa Fenerbahce Martin Skrtel, 34, wakati wa dirisha la usajili la mwezi Januari, lakini beki huyo kisiki wa zamani wa Liverpool aliktaa ofa ya miamba hao wa Uhispania. (AS)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents