Michezo

Taarifa za usajili barani Ulaya, Marcos Rojo kung’olewa United, Jovic awindwa na AC Milan

Taarifa za usajili barani Ulaya, Marcos Rojo kung'olewa United, Jovic awindwa na AC Milan

Klabu ya Uturuki ya Fenerbahce inataka kumsaini beki wa Manchester United na Argentine Marcos Rojo, 29, kwa mkopo . (A Spor, via Manchester Evening News). Borussia Dortmund imeongeza maradufu mshahara wa kinda wa miaka 19 wa England Jadon Sancho hadi £80,000 kwa wiki ili kuzuia klabu nyengine kumwania. (Bild – in German)

Klabu za ligi ya Premia Manchester City, Tottenham na Arsenal zinamchunguza kinda wa Renne mwenye umri wa miaka 16 Eduardo Camavinga ambaye aliiongoza klabu hiyo kuilaza PSG 2-1 katika ligi ya daraja la kwanza Ufaransa siku ya Jumapili. (Mail)

Luca Jovic

Mchezaji mpya wa Real Madrid Real Luka Jovic huenda akajiunga na AC Milan kwa mkopo miezi miwili tu baada ya mshambuliaji huyo ,mwenye umri wa miaka 21 kukamilisha uhamisho wa dau la £62m kuelekea katika klabu hiyo ya Uhispania. (Gazzetta, via Sport Bible)

Monaco imekubali kumsaini kiungo wa kati wa Gabon na Southamptoon Mario Lemina 25 kwa mkoipo wa muda mrefu huku ikiwa na fursa ya kumnunua kabisa.. (RMC – in French)

Liverpool imekataa mwenendo wa klabu ya Denmark Nordsjaelland kumchukua mshambuliaji Bobby Duncan, 20, kwa mkopo wa muda mrefu. (Mail)

Georges Kevin N'koudou

Besiktas imekubali makubaliano ya muda mrefu na klabu ya Tottenham kuhusu winga wa Ufaransa Georges Kevin N’koudou. (TRT Spor – in Turkish)

Klabu ya Ubelgiji ya Bruges inataka kumsaini kiungo wa kati wa Tottenham raia wa Kenya Victor Wanyama, 28. (Express)

Nahodha wa zamani wa klabu ya Manchester City Vincent Kompany amekosolewa kwa kujaribu kuiga mbinu za ukufunzi wa Pep Guardiola baada ya kushindwa mechi zake nne za kwanza kama mkufunzi mchezaji na klabu ya Anderlecht. (Mirror)

Mkufunzi wa Anderlecht Vincent Kompany

Juventus iko tayari kumjumuisha aliyewkuwa kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can, 25,miongoni mwa mkataba kuwasaidia kumsaini mchezaji wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic 31. (Tuttosport, via Mail)

Mkufunzi wa zamani wa Ujerumani Berti Vogts amehoji uhamisho wa kiungo wa zamani wa Barcelona kuelekea Bayern Munich , akisema kwamba mchezaji huyo wa Brazil huenda hana uwezo wa kuwa nyota kama alivyokuwa siku za nyuma. (Goal)

Nahodha wa Ufaransa Hugo Lloris ameitaka Tottenham kuonyesha ukakamavu wa hali ya juu msimu huu huku ikitarji kushinda kombe la kwanza tangu 2008. (Standard)

Phillipe Countinho

Klabu ya Birmingham City imehusishwa na uhamisho wa beki wa kushoto wa Uhispania mwenye umri wa miaka 22 Alberto Redondo, ambaye aliachiliwa na Getafe mwisho wa msimu uliopita. (Footmercato, via Birmingham Mail)

Everton inapanga kucheza bila mashabiki mechi ya kirafiki ili kuwasaidia baadhi ya wachezaji wake wapya kuimarisha mchezo wao.. (Liverpool Echo)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents