Technology

Taarifa zenu binafsi zinahitajika Whatsapp na Facebook

WhatsApp inawalazimisha watumiaji wake kukubali iwasilishe maelezo yao binafsi kwa Facebook ikiwa wanataka kuendelea kutumia huduma hiyo.


Kampuni hilo inawaonya watumiaji kupitia taarifa zinazotolewa kwenye simu zao zinazosema “unahitajika kuruhusu agizo hili ili kuendelea kutumia WhatsApp” – au wafute akaunti zao.

Lakini Facebook, ambayo inamiliki WhatsApp, imesema watumiaji wa mtandao huo waliyopo Ulaya na Uingereza hawataathiriwa na muongozo huo na watahitajika kukubali masharti mapya.

Hatua hiyo imeungwa mkono na baadhi ya watu wakisema ni ushindi kwa wasimamizi wa faragha wa EU.

Muda wa mwisho wakukubali mabadiliko hayo mapya katika maeneo hayo ni Februari 8, na baada ya hapo “utahitajika kukubali agizo hilo ili kuendelea kutumia WhatsApp”, kampuni hiyo ilisema katika taarifa zinazowasilishwa kwa watumiaji.

Sehemu ya sera ya faragha ya kimataifa ya awali ambayo ilikuwa inawasihi watumiaji kukubali maelezo yao kuwasilishwa kwa Facebook kwa hiari katika siku 30 za kwanza imeondolewa baada ya mabadiliko haya mapya kuanza kutekelezwa.

Badala ya katika maagizo ya hivi punde, watumiaji wanaelekezwa sehemu ya kutafuta msaada mtandaoni “ikiwa wangelipendelea kufuta akaunti zao”.

Hatua hiyo imewafanya baadhi ya watu mitandaoni – akiwemo mwanzilishi wa Tesla na SpaceX Elon Musk- kutoa with kwawatumiaji wa mtandao huo kujiunga na huduma zingine za ujumbe wa faragha kama Signal na Telegram.

Kutojumuishwa kwa Ulaya

Awali kulikuwa na mkanganiyiko kuhusu jinsi ya hatua hiyo itawaathiri watumiaji wa Ulaya na Uingereza.
Muktasari wa ”maelezo muhimu” ya mabadiliko hayo mapya yatajumuishwa na Facebook kimataifa – lakini hatua hiyo haijajumuishwa katika huduma sawa na hiyo kwa watumiaji wa mtandao huo yaliyopo Ulaya.
Baadaye Alhamisi, Facebook ilitoa taarifa ikisema kwamba mabadiliko hayo hayahusu” eneo la Ulaya” – ambayo inajumuisha EU, EEA na Uingereza baada ya -Brexit.

“Ili kuondoa shaka, katika mpango huu mpya WhatsApp haiwasilishi data ya watumiaji wake wa maeneo ya Ulaya kwa Facebook kwa lengo la Facebook kutumia data hiyo kujiimarisha au kwa ajili ya biashara” msemaji alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents