Afya

Taasisi ya Saratani ya Ocean Road yapokea msaada kutoka Benki ya NIC Tanzania

Benki ya NIC Tanzania yatoa msaada katika Taasisi ya Saratini ya Ocean Road(ORCI) Dar es Salaam, 8th Machi,2019,  Benki ya NIC Tanzania leo imeadhimisha siku ya wanawake duniani inayosherehekewa kote duniani tarehe 8 Machi kwa kutembelea na kutoa msaada katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road(ORCI).

Akiongea katika tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania, Margaret Karume alisema, “Siku ya wanawake duniani ni siku kubwa katika kalenda ya wafanyakazi wa benki hii, kwa ajili ya kusaidia na kuyainua maisha ya wanawake wasiojiweza katika jamii iliyotuzunguka. Saratani ni  ugonjwa ambao umeathiri na unaendelea kuathiri watanzania wengi sana, Zaidi kama haijagundulika mapema”.

Aliongeza kwa kusema, kila mmoja wetu ananafasi ya kucheza katika jamii, ambapo dunia inahitaji usawa. Katika uamuzi wetu wa kutoa msaada kwa wagonjwa wa saratani, tujenga usawa kwa ajili yakuwa na dunia iliyobora.


“Kama Benki, tumejikita kuhakikisha tunatoa mchango chanya, kwa jamii tunazo endesha shughli zetu. Ndio sababu kusaidia Taasisi kama hizi ipo katika mkakati maalum wa kusaidia jamii,” alisema Karume.


Akiongea katika hafla hiyo Afisa Ustaei wa Taasisi hiyo Malkiory Niniko alisema, “Tunaipongeza Benki ya NIC Tanzania, kwa kutoa msaada huu, na tunawaomba wadau mbalimbali waige mfano huu adhimu, na Taasisi inakaribisha usaidizi kutoka idara mbalimbali kwa sababu haiwezi kufanikisha malengo yake yote kwa mkupuo”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents